Mkutano wa NATO wafanyika nchini Uturuki

Martin Mwanje
1 Min Read
Picha kwa hisani ya RFI

Rais wa Marekani Donald Trump ni miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa Umoja wa Kujihami wa Nchi za Kaskazini mwa Atlantiki, NATO unaoandaliwa nchini Uturuki.

Uhusiano kati ya Marekani na umoja huo haujakuwa mzuri katika siku za hivi karibuni.

Mkutano huo unaanza leo Jumanne katika mji mkuu wa Ankara.

Trump amekuwa mstari wa mbele kuikosoa NATO kuhusiana na matumizi ya ulinzi,akizitaka nchi wanachama kutoa mchango zaidi wa fedha kwa umoja huo.

Mwezi jana, alimwambia Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte kuwa anataka uaminifu zaidi kutoka kwa umoja huo.

Rutte ameonekana kupinga shinikizo la Marekani akisema nchi  wanachama wa NATO zianaendelea kuziba pengo la matumizi.

Aidha, aliashiria kuwa nchi wanachama wa NATO zitatangaza makumi ya mabilioni ya dola katika mikataba mipya wakati wa mkutano huo wa siku mbili unaoanza leo Jumanne.

 

Share This Article