Waombolezaji zaidi ya milioni 10, pamoja na jumbe kutoka mataifa zaidi ya 100, wanatarajiwa kumiminika jijini Tehran leo, kuhudhuria mazishi ya kitaifa ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.
Mazishi hayo yanafuatia kuuawa kwa kushtua kwa Khamenei pamoja na baadhi ya wanafamilia wake, mwanzo za vita vikali vya Marekani ikishirikiana na Israel dhidi ya Iran.
Tukio hilo limebadili kwa kiasi kikubwa mwelekeo wa siasa za kijiografia duniani.
Mamlaka zimetangaza siku kadhaa za maombolezo ya kitaifa, huku usalama ukiimarishwa katika mji mkuu wakati viongozi wa dunia, mawaziri wa mambo ya nje na maafisa waandamizi wanajiandaa kuhudhuria shughuli hiyo.
Vyombo vya habari vya serikali ya Iran vimeeleza mazishi hayo kuwa mkusanyiko mkubwa zaidi wa umma kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo, huku misafara ya waombolezaji ikienea katikati ya Tehran.
Mamilioni ya wananchi nao watajipanga kandokando ya barabara kutoa heshima zao za mwisho.
Viongozi wa kidini wametoa wito wa umoja, huku viongozi wa serikali wakiahidi kuwa taifa litaendelea kuwa imara licha ya kumpoteza kiongozi wake wa ngazi ya juu kabisa.
Mauaji hayo yameongeza hofu ya kuzuka kwa mzozo mpana zaidi wa kikanda na kuchochea juhudi za haraka za kidiplomasia ili kuzuia hali hiyo isizidi kuwa mbaya.
Wachambuzi wanasema mazishi hayo huenda yakawa ishara ya nguvu ya mshikamano wa kitaifa na wakati muhimu katika mgogoro unaoendelea, huku macho ya dunia yakielekezwa Tehran.