Kiungo wa Senegal Pape Gueye ameapa kuwa kamwe hatarudi kuichezea timu hiyo endapo benchi ya kiufundi haitabadilishwa.
Gueye alisema haya Jumatano usiku ya Kombe la Dunia, baada ya mechi yao ya awamu ya 32 waliposhindwa 3-2 na Ubelgiji.
Simba wa Teranga walikuwa wakiongoza mabao 2-0 kufikia dakik ya 85, kabla ya makosa ya walinzi kuwaruhusu Ubelgiji, kukomboa magoli yote ndani ya muda wa sekunde 61, na kisha wakapata bao la ushindi kupitia penati ya dakika ya 125 yake Youri Tielemans.
Wadadisi wengi wamemshutumu kocha wa Senegal Pape Thiaw, kwa mabadiliko matatu aliyofanya yaliyofifisha timu na kuwapa Ubelgiji fursa ya kurejea mchezoni na baadaye kuwabandua nje muda mfupi, kabla ya kipenga cha mwisho.
Senegal walicheza hadi robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2002, na kubanduliwa nje katika hatua makundi mwaka 2018, na hatimaye kucheza hadi raundi ya 16 mwaka 2022.