Nahodha na mshambulizi wa timu ya Argentina Lionel Messi angali kuongoza chati ya ufungaji magoli katika makala ya 23 ya dimba la Kombe la Dunia linaloandaliwa kwa pamoja na Canada, Mexico na Marekani.
Messi amefunga mabao 6, akiweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika kila fainali za Kombe la Dunia alizoshiriki huku pia akiweka rekodi mpya ya kufunga mabao 19 akiwa mfungaji bora tangu kuanza kwa kipute hicho mwaka 1930.
Mechi 72 za hatua ya makundi zimekamilika na magoli 215 kufungwa, idadi wastani ya mabao 2.99 kwa kila mechi.