Rais wa China atoa wito wa hatua thabiti katika kilimo cha kisasa na maeneo ya vijijini

radiotaifa
1 Min Read
Rais Xi akiwa na maafisa wengine wakati wa ziara ya ukaguzi mjini Dezhou, mkoa wa Shandong, mashariki mwa China

Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa hatua thabiti kuchukuliwa ili kuendeleza kilimo cha kisasa na maeneo ya vijijini.

Rais Xi aliyasema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi mjini Dezhou, mkoa wa Shandong, mashariki mwa China.

Amesema juhudi zinapaswa kufanyika kuimarisha uwezo wa jumla wa uzalishaji, ubora, na utendaji wa kilimo ili kuhakikisha usambazaji thabiti wa bidhaa muhimu za kilimo kama nafaka, kujenga maeneo mazuri na masikilizano vijijini kwa watu kuishi na kufanya kazi kuendana na mazingira husika.

Pia ametoa wito wa wakulima kuongozwa kujenga maisha mazuri kupitia kufanya kazi kwa bidii na busara.

Taarifa ya CGTN 

Share This Article