Timu 16 zafuzu awamu 32 Kombe Dunia

Timu zilizofuzu kwa kuwa katika nafasi za tatu bora kwenye makundi yao ni Uswdi,Bosnia Herzegovina na Ecuador.

Dismas Otuke
1 Min Read

Jumla ya timu 16 zimejikatia tiketi kwa awamu ya 16 bora kuwania Kombe la Dunia huku nafasi nyingine 16 zikisalia.

Timu zilizofuzu baada ya kumaliza katika nafasi mbili bora za makundi ni Mexico, Ivory Coast kutoka kundi A, Uswizi na Canada kutoka kundi B, na Morocco na Brazil za kundi C.

Mataifa mengine yaliyoingia mchujo huo ni Marekani, Autsralia za kundi D, Ujerumani na Ivory Coast za kundi E na Uholanzi na Japani za kundi F.

Timu zilizofuzu kwa kuwa katika nafasi za tatu bora kwenye makundi yao ni Uswdi, Bosnia Herzegovina na Ecuador.

Nafasi 16 za mwisho zitajazwa kufikia mapema Jumapili hii wakati wa mechi za mwisho hatua ya makundi.

Share This Article