Timu sita zafuzu kwa awamu ya 32 bora,Kombe la Dunia

Mataifa mengine yaliyofuzu baada ya kushinda mechi mbili za kwanza ni ;Ujerumani ya kundi E,Ufaransa na Norway za kundi I,na Argentina kutoka kundi J.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu sita zimejikatia tiketi kwa raundi ya 32 bora ya makala ya 23 ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini mexico,Canada na Marekani.

Wenyeji wenza Mexico na Marekani kutoka makundi ya A na D wamefuzu baada ya kujihakikishia nafasi ya kwanza yao mtawalia.

Mataifa mengine yaliyofuzu baada ya kushinda mechi mbili za kwanza ni ;Ujerumani ya kundi E,Ufaransa na Norway za kundi I,na Argentina kutoka kundi J.

Timu mbili bora kutoka kila kundi na timu nane zitakazomaliza ,atika nafasi za tatu bora kutka makundi yote zitajumuisha mataifa 32 yatakayoshiriki awamu ya 32 bora.

Share This Article