Misri yawakamata washukiwa wa uhalifu karibu na mpaka wa Sudan

Miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na raia 136 wa kigeni na 87 wa Misri, wanaoshukiwa kuhusika na uhalifu wa mipakani na uchimbaji haramu wa dhahabu.

Tom Mathinji
1 Min Read
Misri yawakamata washukiwa 223 wa uhalifu karibu na mpaka wa Sudan.

Jeshi la Misri limesema limewakamata washukiwa 223 wa uhalifu kwenye operesheni ya kiusalama karibu na mpaka wa nchi hiyo na Sudan.

Kulingana na jeshi hilo, miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na raia 136 wa kigeni na 87 wa Misri, wanaoshukiwa kuhusika na uhalifu wa mipakani na uchimbaji haramu wa dhahabu.

Kwenye taarifa iliyotolewa na jeshi hilo, operesheni hiyo ililenga maeneo yanayoaminika kukaliwa na makundi ya wahalifu, wanaohusika na ulanguzi wa silaha na mihadarati, biashara haramu ya dhahabu na uhamiaji kinyume na sheria.

Aidha, jeshi hilo lilisisitiza kuwa shughuli hizo ziliibua moja kwa moja tisho kwa usalama wa kitaifa wa Misri, na kuathiri vibaya udhabiti wa uchumi, uwekezaji na juhudi za maendeleo endelevu.

Wanajeshi hao pia walipata magari 14, vifaa vya mawasiliano na pesa taslimu za zikiwemo sarafu za kigeni, pamoja na silaha na risasi.

Mashini na vifaa vya uchimbaji haramu wa dhahabu zipia zilitwaliwa.

 

TAGGED:
Share This Article