MCA, wengine wawili wakamatwa kwa kumiliki bunduki haramu Nairobi

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), imesema bastola hiyo ilikuwa ikimilikiwa bila leseni halali.

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa watatu wakamatwa na bunduki haramu Nairobi.

Washukiwa watatu, akiwemo mwakilishi wadi (MCA), wanazuiliwa na polisi baada ya kupatikana na bunduki haramu kwenye operesheni iliyotekelezwa na polisi katika eneo la Roasters, Nairobi.

Watatu hao Patrick Karani, ambaye ni mwakilishi wadi katika eneo bunge la Embakasi, Stephen Kimathi Karimoni na Stanley Njogu Irungu, walitiwa nguvuni kwenye afisi ya mwakilishi wadi huyo, baada ya polisi kuwafumania na kupata bastola aina ya Glock ikiwa na risasi 12.

Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kwenye ukurasa wa X imesema kuwa bastola hiyo ilikuwa ikimilikiwa bila leseni halali.

“Huku bastola hiyo na risasi zikihifadhiwa kama ushahidi, watatu hao wanazuiliwa wakisubiri kufikishwa mahakamani,” ilisema DCI.

Kulingana na DCI, umiliki haramu wa bunduki ni hatari kwa usalama wa umma, ikionya kuwa watakaopatikana na silaha hiyo bila leseni watachukuliwa hatua za kisheria.

TAGGED:
Share This Article