Kenya itashirikiana na Benki ya Dunia kuchochea ukuaji, asema Rais Ruto

Rais Ruto alikaribisha mageuzi ya Benki ya Dunia kwenye mfumo wa fedha wa Kimataifa utakaopanua upatikanaji wa fedha na kuimarisha matarajio ya mataifa yanayostawi.

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto na Rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga nchini Ufaransa.

Rais William Ruto amesema Benki ya Dunia imekuwa mshirika muhimu kwa maendeleo ya Kenya, huku ikipiga jeki uwekezaji ambao unaimarisha maisha na unaopanua fursa za kiuchumi.

“Tunapoboresha ajenda ya maendeleo yetu ya maendeleo, Kenya itaendelea kushirikiana kwa karibu na Benki ya Dunia kuchochea ukuaji na kufanikisha matokeo bora kwa watu wetu,” alisema kiongi huyo wa taifa.

Aliyasema hayo aliposhiriki mazungumzo na Rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga, pembezoni mwa mkutano wa kundi la G7 Jijini Évian, Ufaransa.

Kwenye mkutano huo, viongozi hao wawili walijadili vipaumbele kwa maendeleo ya Kenya na uwekezaji utakaosababisha ukuaji endelevu na wa pamoja.

Aidha, Rais Ruto alikaribisha mageuzi ya Benki ya Dunia kwenye mfumo wa fedha wa Kimataifa utakaopanua upatikanaji wa fedha na kuimarisha matarajio ya mataifa yanayostawi.

Rais Ruto anawakilisha Afrika kwenye mkutano huo wa G7, kwa mwaliko wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Share This Article