Makala ya 23 ya kindumbwendumbwe cha Kombe la Dunia yataingia siku ya pili leo, huku waandalizi wenza Canada na Marekani wakicheza mechi za ufunguzi.
Canada watawaalika Bosnia Herzegovina katika uwanja wa Toronto kuanzia saa nne usiku.
Mechi hiyo itatanguliwa na sherehe za ufunguzi sawia na zile zilizofanyika nchini Mexico siku ya Alhamisi.
Baadaye saa kumi alfajiri kesho itakuwa zamu ya Marekani kuandaa sherehe za ufunguzi na mechi ya kwanza ya kundi D, kati ya Marekani na Paraguay .
Mchuano huo utasakatwa katika uwanja wa Los Angeles.
Jumla ya mechi 104 zitachezwa katika makala ya mwaka huu yanayoshirikisha mataifa 48 kwa mara ya kwanza.