Timu ya taifa ya wanawake ya Kenya itakabiliana na Lesotho, leo alasiri katika mechi ya kirafiki katika uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia.
Harambee Starlets wanaotumia mechi hizo kujinoa kwa kipute cha kombe la mataifa ya Afrika WAFCON,watakuwa wakicheza mechi ya pili baada ya kutoka sare ta bao moja na Zambia wiki jana.
Kenya imejumuishwa kundi A katika fainali za WAFCON kati ya Julai 26 na Agosti 16, pamoja na Algeria,Senegal na Morocco.
Pambano la Kenya na Lesotho litang’oa nanga saa kumi alasiri.
Kenya watashiriki WAFCON kwa mara ya pili baada ya kushiriki mwaka 2016.