Kiongozi wa Mashtaka wa ICC Karim Khan asimamishwa kazi

Khan anadaiwa kumdhulumu kimapenzi mfanyakazi wa kike wa ICC mwaka 2024, madai ambayo ameyakanusha vikali.

Tom Mathinji
1 Min Read
Karim Khan- Kiongozi wa Mashtaka ICC.

Kiongozi wa Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Karim Khan amesimamishwa kazi kutokana na madai ya dhuluma za kingono.

Bodi ya mahakama ya ICC ilitangaza kwamba hatua ya kumsimamisha kazi Khan imetokana na ushahidi na mapendekezo ya ripoti iliyochunguza nadai dhidi yake.

Khan anadaiwa kumdhulumu kimapenzi mfanyakazi wa kike wa ICC mwaka 2024, madai ambayo ameyakanusha vikali.

Hata hivyo, uamuzi wa mwisho kuhusu  iwapo Khan ataondolewa kabisa kwenye wadhifa huo, utafikiwa wakati wa kikao maalumu cha nchi wanachama wa mkataba ulioanzisha mahakama hiyo yenye makao yake mjini The Hague nchini Uholanzi.

Khan ambaye aligonga vichwa vya habari duniani kwa kuomba hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na viongozi wengine kuhusiana na mzozo wa Gaza, amekuwa likizoni tangu mwezi Mei mwaka 2025, kutoa fursa kwa uchunguzi kufanywa kuhusiana na madai hayo.

TAGGED:
Share This Article