Mahakama Kuu Kenya,yadumisha kutimuliwa kwa Gachagua

Hata hivyo, ilikuwa afueni ndogo baada ya Mahakama kumpa Gachagua ridhaa ya shilingi milioni 50 kufuatia kukiukwa kwa haki zake wakati wa mchakato wa kumuengua afisini.

Dismas Otuke
1 Min Read
Rigathi Gachagua.

Mahakama Kuu ya Kenya imedumisha kutimuliwa kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua .

Katika uamuzi wa Jumatatu Majaji watatu wanaoskiza kesi hiyo ya mwaka 2024 walisema bunge la kitaifa lilifuata utaratibu ufaao chini ya katiba ya sasa.

Majaji hao walisema katiba ya sasa haina njia mbadala wa kubadilisha kutimuliwa afisini na mahakama haina uwezo wa kubatilisha uamuzi wa kung’atuliwa baada ya Naibu Rais mpya kuteuliwa.

Aidha,Mahakama ilibaini kuwa bunge lilikiuka haki za Gachagua ,kwa kuendelea mbele na hoja ya kumng’atua licha kulazwa hospitalini.

Hata hivyo mahakama ilisema kuwa hilo pekee halingetosha kubadili kutimuliwa kwake.

Pia Mahakama ilibaini kuwa uteuzi wa Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais ,uliifuata utaratibu unaofaa kikatiba.

Hata hivyo ilikuwa afueni ndogo baada ya Mahakama kumpa Gachagua, ridhaa ya shilingi milioni 50, kufuatia kukiukwa kwa haki zake wakati wa mchakato wa kumuengua afisini.

Share This Article