Baraza jipya la Mawaziri nchini Uganda limeapishwa katika hafla iliyoongozwa na Rais Yoweri Museveni, siku ya Jumatatu katika Ikulu ya Entebe.
Mawaziri 78 waliapishwa huku wanne walio na uraia pacha wakikosa kujitokeza.
Mawaziri wateule waliokosa uapisho ni Adonia Ayebare wa Mashauri ya kigeni,Shartsi Musherure wa mashirika madogo ya kifedha,Calvin Echodu wa mambo ya ndani,na Lawrence Muganga wa idara ya mambo ya ndani.
Licha ya Wabunge kuwaidhinisha Mawaziri hao wanne, yamkini walikuwa hawajatatua swala la uraia pacha.