Makala ya tano ya mbio za kila mwaka za Nairobi City Marathon yameanzishwa rasmi mapema Jumapili na Waziri wa Michezo Salim Mvurya nje ya City Hall.
Mbio hizo zilizo na vitengo vinne vya marathon, nusu marathon, kilomita 10 na kilomita 5, zimewashirikisha wanariadha zaidi ya 17,000.
Washindi wa marathon watatuzwa shilingi milioni 3.5, nafasi ya pili milioni 2.25 na nafasi ya tatu milioni 1.5.
Lengo la mbio hizo ni kutangaza jiji la Nairobi.