Watu zaidi ya 40 wafariki kwa kiu katika jangwa la Sahara

Kulingana na mamlaka, watu hao walikuwa kwenye Kundi  lililokuwa likirejea kutoka Mali baada ya kuhudhuria sikukuu ya Kiislamu.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu zaidi ya 40 wafariki kwa kiu kwenye jangwa la Sahara.

Watu zaidi ya 40 wamefariki kwa kiu katika Jangwa la Sahara kaskazini mwa Niger,  baada ya lori walimokuwa wakisafiria kuharibika.

Kulingana na mamlaka, watu hao walikuwa kwenye Kundi  lililokuwa likirejea kutoka Mali baada ya kuhudhuria sikukuu ya Kiislamu wakati walipoishiwa maji, wakati gari hilo lilipokwama kilomita  80 magharibi mwa Assamaka, kituo kikuu cha mpakani kati ya Niger na Algeria.

Kwenye taarifa kutoka kwa afisi ya Gavana wa eneo la Agadez ilisema watu wawili pekee ndio walinusurika, wakitembea zaidi ya kilomita 50 kuvuka jangwa hadi Assamaka, ambako walizitaarifu mamlaka.

“Walikosa maji na kushindwa kulikarabati gari hilo, wasafiri hao walijipata kwenye mazingira magumu kutokana na kiwango cha juu zaidi cha joto,” ilisema afisi hiyo.

“Miili kadhaa ilipatikana chini ya lori lisilosogea na maeneo yaliyolizunguka.”

Jangwa hilo linafahamika sana kwa usafiri wa wakimbizi na wahamiaji ambao wanatoroka Afrika kuingia bara Uropa, wengi wakifariki kutokana na kiu na ukosefu wa chakula.

Share This Article