Timu ya taifa ya soka ya wanaume ya Kenya – Harambee Stars, itachuana na Lesotho leo alasiri katika mchuano wa kwanza wa kimataifa wa kirafiki mjini Pretoria, Afrika Kusini.
Kenya inayofunzwa na Benni McCarthy itacheza pambano la marudio Juni 7 kabla ya kurejea nyumbani.
Stars wanatumia mechi hiyo kujiandaa kwa michuano ya makundi kufuzu kwa fainali za AFCON zitakazoandaliwa na Kenya, Uganda na Tanzania, ndani ya miezi 12 ijayo.
Kenya na Lesotho wanamenyana leo kwa mara ya nne katika historia, Lesotho wakiibuka kidedea mechi moja, nazo mbili kumalizikia sare kati ya mwaka 2013 na 2014.