Timu ya Kenya ya akina dada chini ya umri wa miaka 17, imefuzu kwa raundi ya tatu na ya mwisho ya kutafuta tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia baada ya kuibandua Uganda.
Kenya ilifuzu kwa raundi ya tatu baada ya sare tasa dhidi ya Uganda katika mechi ya marudio ya raundi ya pili katika uwanja kitaifa wa Nyayo.
Rising Starlets ilifuzu kwa bao la ugenini baada ya duru ya Kwanza kumalizikia sare ya bao moja mjini Kampala wiki Jana.