Wanafunzi kadhaa wa Utumishi Girls wahofiwa kufariki katika mkasa wa moto

Wengi wa wanafunzi walishindwa kujinusuru baada ya milango ya bweni kukataa kufunguka.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanafunzi kadhaa wanahofiwa kufariki kwenye mkasa wa moto ulioteketeza bweni la shule ya Utumishi Girls Academy  Senior School,mjini Gilgil, kaunti ya Nakuru, mapema Alhamisi.

Yamkini moto huo ulizuka mida ya saa tisa unusu Alfajiri, wakati wanafunzi walikuwa wamelala kwenye bweni.

Wengi wa wanafunzi walishindwa kujinusuru baada ya milango ya bweni kukataa kufunguka.

Shirika la Msalaba Mwekundu, limetenga kituo cha kuwasaidia majeruhi na kutoa kutoa ushauri nasaha.

Wanafunzi wengine kadhaa waliojeruhiwa  wanapokea matibabu  katika Hospitali ya St. Joseph.

Chanzo cha moto huo hakijulikani huku uchunguzi ukiendeshwa na maafisa wa Polisi.

 

Share This Article