Congo kuondoa VIZA kwa wageni wa Afrika kuanzia Januari mosi

Congo ni ya hivi punde kuondoa viza kwa wageni ikijiunga na Kenya,Rwanda,Ushelisheli na Togo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Congo imetengaza kuondoa hitaji la Viza ya usafiri kwa wageni wote wanaotokea barani Afrika, kuanzia Januari mosi mwaka 2027, ili kurahisisha usafiri.

Kulingana na rais Denis Sassou Nguesso, hatua hiyo itaongeza utangamano wa kikanda na kuhuisha biashara .

Hali hiyo itafanya kuwa rahisi kwa watalii na wageni wa kutoka barani Afrika wanaonuia kuzuru Congo, aidha kwa biashara au kitalii.

Congo ni ya hivi punde kuondoa viza kwa wageni ikijiunga na Kenya,Rwanda,Ushelisheli na Togo.

Umoja wa Afrika unapendekeza kuondolewa kwa viza kwa wageni wa Afrika wanaozuru mataifa menhinge barani ifikiapo mwaka 2063, ili kurahisha biashara na kutembea kutoka mpaka hadi mwingine.

TAGGED:
Share This Article