Majeshi ya Nigeria yamewaokoa raia 92 ,waliokuwa wametekwa nyara na kundi haramu la Boko Haram.
Maafisa hao wa polisi walisema waliendesha oparesheni chini ya uangalizi mkali katika maeneo yanayotawaliwa na wanamgambo hao.
52 kati ya mateka hao ni wanaume huku wengine 33, wakiwa wanawake na watoto saba.
Hata hivyo wanajeshi hao hawajasema muda ambao mateka hao walikuwa mikononi mwa Boko Haram.