Mamelodi wapige gwaride la ubingwa Afrika Kusini

Kwenye gwaride hilo wachezaji na maafisa wa Mamelodi walitangamana na kusheherekea ubingwa huo huku wakibeba kombe.

Dismas Otuke
1 Min Read

Washindi wa Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika Mamelodi Sundowns, wameendelea na gwaride lao katika miji kadhaa ya Afrika Kusini siku ya Jumanne kusheherekea taji ya pili.

Mamelodi walinyakua taji ya Afrika kwa mara ya pili Jumapili iliyopita baada ya kuwashinda AS FAR,ya Morocco mabao 2-1.

Ilikuwa maya ya kwanza kwa Mamelodi kutwaa kombe hilo tangu mwaka 2016.

Kwenye gwaride hilo wachezaji na maafisa wa Mamelodi walitangamana na kusheherekea ubingwa huo na mashabiki huku wakibeba kombe.

Ushindi huo unawawezesha Mamelodi kufuzu kuiwakilisha Afrika katika Kombe la Dunia mwaka 2029.

Share This Article