Maafisa wa Shirikisho la Riadha Ulimwenguni wazuru Kenya

Kenya ilikuwa mwenyeji wa mashindano ya Dunia kwa wanariadha chipukizi chini ya umri wa miaka 18 mwaka 2017, na yake ya chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2021.

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa Shirikisho la Riadha Ulimwenguni wamezuru Kenya siku ya Jumanne, katika ziara ya kutathmini maombi ya Kenya Kuandaa mashindano ya Dunia ya mwaka 2029, au yale ya mwaka 2031.

Ujumbe huo uliongozwa na Mwanachama wa Baraza Kuu la shirikisho la Riadha Ulimwenguni Antti Pihlakoski .

Akizungumza kwenye kikao hicho Katibu katika Wizara ya Michezo Elijah Mwangi, alikariri kujitolea kwa Kenya, kuandaa mashindano ya hadhi ya kimataifa endapo  itatwikwa jukumu hilo.

Kenya ilikuwa mwenyeji wa mashindano ya Dunia kwa wanariadha chipukizi chini ya umri wa miaka 18 mwaka 2017, na yale ya chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2021.

Ujumbe huo uliozuru Kenya pia ulijumuisha Mkurugenzi wa mashindano Marton Gyulai,Msimamizi wa maombi ya kuandaa mashindano Mark Hurst na Niels Lindholm,pamoja na afisa wa utekelezaji Nigel Swinscoe.

Share This Article