FIFA World CUP 2026 :Timu 39 kupiga kambi Marekani

Fainali itachezwa Julai 19 ,katika uwanja wa Metlife,katika jimbo la New York.

Dismas Otuke
1 Min Read

Jumla ya mataifa 39 yatakayoshiriki fainali za 23, za Kombe la Dunia mwaka huu yatakita kambi ya mazoezi nchini Marekani.

Timu nyingine saba zitakita ya mazoezi  nchini Mexico, huku mengine mawili  yakiwa Canada.

Kipute cha Kombe la Dunia kitaandaliwa kati ya Juni 11 na Julai  19, huku jumla ya mechi 104 zikichezwa katika miji 16 tofauti.

Marekani itaandaa mechi 78, huku Canada na Mexico, zikigawana mechi 13 kila moja.

Fainali itachezwa Julai 19 ,katika uwanja wa Metlife,katika jimbo la New York.

 

Share This Article