Ahmadou Al Aminou Lo ateuliwa Waziri Mkuu mpya wa Senegal

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye

Rais Bassirou Diomaye Faye wa Senegal, amemteua Ahmadou Al Aminou Lo kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.

Tangazo la kuteuliwa kwa Waziri mkuu huyo mpya, zilitolewa na Katibu Mkuu wa Ikulu kupitia Televisheni ya taifa Jumatatu Mei 25, 2026.

Awali Ahmadou Al Aminou Lo ambaye ni mtaalam wa maswala ya uchumi, ​alihudumu katika Benki Kuu ya Senegal katika mataifa ya Magharibi mwa Afrika.

Akitoa hotuba yake kupitia Televisheni ya Taifa baada ya uteuzi wake, Lo alikiri kuwepo kwa changamoto ya kiuchumi nchini Senegal ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa bei ya nishati, mvutano wa kijamii na kuzorota kwa mazingira ya usalama wa kikanda n.k.

Alisema serikali ya Senegal itahimiza sera mbalimbali za umma kwa kuzingatia Ruwaza ya 2050 ya Senegal, na kuendelea kuitekeleza ajenda hiyo ya mageuzi ya nchi.

Faye alimfurusha aliyekuwa Waziri Mkuu  ​Ousmane Sonko siku ya Ijumaa baada ya miezi kadhaa ya taharuki kushuhudiwa nchini humo.

Share This Article