Serikali yatangaza Mei 27 kuwa siku kuu ya Eid al-Adha

Siku kuu hiyo huadhimishwa na Waislamu kuashiria kukamilika kwa safari ya Hajj mjini Mecca.

Dismas Otuke
0 Min Read
Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen.

Serikali imetangaza Jumatano hii Mei 27, kuwa siku kuu ya Eid al-Adha,hivyo basi kuwa siku ya mapumziko.

Siku kuu hiyo huadhimishwa na Waislamu kuashiria kukamilika kwa safari ya Hajj mjini Mecca.

Eid- Al- Adha ni sherehe ya kumbukumbu ya kafara ya mtoto aliyotoa Mtume Abraham, kwa Mungu kuashiria heshima yake.

Siku hii husherekewa na Waislamu kwa kuchinja mifugo na kugawana nyama na wasiojimudu katika jamii.

Share This Article