Ubalozi wa Marekani jijini Dares Salaam, Tanzania, umetoa tahadhari ya usafiri kutokana na hofu ya ugonjwa wa Ebola.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya Habari, Ubalozi huo umesema tangazo hilo linafuatia hatua zilizochukuliwa na wizara ya afya Tanzania, ya kuweka ulinzi mkali mipakani, ili kuzuia msambao wa ugonjwa huo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Pia Ubalozi hupo umeshauri kuwa raia wake ambao wamekuwa DRC au Sudan Kusini kwa siku 21, zilizopita ni sharti waingie Marekani, kupitia uwanja wa kimataifa ndege wa Washington Dulles, ni sharti wachunguzwe kabla ya kuingia.
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, umewataka raia wake kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya.