Kikosi cha Kenya kwa mashindano ya Riadha Duniani kwa chipukizi chatajwa

Mabingwa wa Cynthia Chepkurui,bingwa wa michezo ya Afrika Emmanuel Lemiso na mshindi wa nishani ya shaba Afrika Joyline Chepkemoi, ni baadhi ya wanariadha waliojumuishwa kikosini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha riadha nchini kimetaja kikosi cha wanariadha 22 watakaoiwakilisha Kenya, kwenye mashindano ya dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mwezi Agosti mwaka huu mjini Oregon,Marekani.

Kikosi hicho kilichotajwa kinawajumuisha wanariadha wenye uzoevu na kiliteuliwa kufuatia majaribio ya kitaifa ya siku mbili yaliyokamilika leo katika uwanja wa Nyayo.

Mabingwa wa Cynthia Chepkurui,bingwa wa michezo ya Afrika Emmanuel Lemiso na mshindi wa nishani ya shaba Afrika Joyline Chepkemoi, ni baadhi ya wanariadha waliojumuishwa kikosini.

Chama cha riadha Kenya kimetaja idadi ndogo ya wanariadha watakaoelekea Marekani kufuatia wengi wao kukosa kuafiki muda wa kufuzu katika mbio za masafa mafupi na yale ya kadri.

Timu hiyo imetajwa mapema ili kutoa muda wa kuandaa stakabadhi za usafiri na kitaripoti kambini kwa mazoezi ,mwezi mmoja kabla ya mashindano ya dunia.

Kenya ilimaliza ya tano katika makala ya mwaka 2024 mjini Lima Peru kwa dhahabu 3 fedha 3 na shaba 1.

Wakati uo huo wanariadha wengine 20, wamechaguliwa kushiriki mashindano ya Afrika mashariki kwa chipukizi chini ya miaka 20, yatakayoandaliwa mjini Arusha,Tanzania kati ya tarehe 5 na 6 mwezi ujao.

Share This Article