Maandamano yameshuhudiwa katika maeneo mbalimbali kote nchini Kenya siku ya Jumatatu, kupinga hatua ya serikali kuongeza bei ya mafuta.
Maandamano hayo yameambatana na mgomo wa kitaifa uliotangazwa na wenye magari ya uchukuzi wa umma .
Waandamanaji wamefunga barabara kwa mawe,kuchoma magurudumu huku wakikabiliana vikali na polisi kwa vitoza machozi.
Mamlaka ya kudhibiti bei ya bidhaa za mafuta ilitangaza wiki jana kuwa bei mpya ya lita moja ya Petroli itakuwa shiljingi 214 na senti 25, ikiwa ongezeko la shilingi 16.65, wakati Dizeli ikipanda kwa shilingi 46 na senti 29, hadi shilingi 242 kwa lita moja.
Tayari wenye magari ya usafiri wa umma walitangaza kuongeza bei za nauli kwa asilimia 50, kuanzia leo ilio kukidhia gharama ya uendeshaji biashara.