Tanzania imetangaza kuanza kuzalisha madini ya chuma kuanzia mwezi Agosti mwaka huu,hatua inayotarajiwa kuipunguzia serikali mzigo mkubwa wa uagizaji bidhaa hiyo kutoka nje.
Shirika la maendeleo Tanzania,NDC,lilisaini mkataba miaka mitatu iliyopita na kampuni ya Fujian Hexingwang Industry Tanzania, wa kuanza kuchimba madini katika Wilaya ya Lidowe ,mkoani Njombe.
Kwenye mkataba huo serikali ya Tanzania itamiliki asilimia 36 ya hisa, huku wananchi wakimiliki asilimia 64.
Punde utakapoanza kutekelezwa fursa kadhaa zitabuniwa ikiwemo nafasi za ajira zaidi ya 6,000, na pia kupunguza gharama ya uagizaji vyuma kwa serikali.
Serikali ya Tanzania hutumia dola za Kimarekani bilioni 1.22, kwa mwaka kuagiza vyuma.