Police Bullets watwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Kenya

Bullets wanaongoza jedwali kwa alama 52 kutokana na mechi 20,pointi 8 zaidi ya Ulinzi Starlets wanaokalia nafasi ya pili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Kenya Police Bullets FC, ndio mabingwa wa Ligi Kuu ya wanawake nchini Kenya, msimu wa mwaka 2025/2026.

Police Bullets wamenyakua taji ya Ligi kuu ya wanawake nchini Kenya siku ya Jumapili baada ya kuwashinda Trinity Starlets bao moja kwa bila.

Bullets wanaongoza jedwali kwa alama 52 kutokana na mechi 20,pointi 8 zaidi ya Ulinzi Starlets wanaokalia nafasi ya pili.

Kibera Soccer na Vihiga Queens zinashikilia nafasi za 3 na 4 kwa alama 37 kila moja.

Share This Article