Rais William Ruto ameituza shule ya Maseno Boys katika kaunti ya Kisumu, shilingi milioni tatu .
Ruto alifichua hayo alipohudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 120 siku ya Jumamosi, tangu kuanzishwa kwa shule hiyo .
Alisema kuwa shilingi milioni moja zitatumika kununua ala za muziki kwa bendi ya shule hiyo, huku kiwango kilichosalia cha shilingi milioni 2 kikitumika kwa mahitaji mengine ya wanafunzi shuleni humo.
Rais alihudhuria hafla hiyo akiwa amevalia koti rasmi la shule hiyo sawia na viongozi wengine waliofika katika sherehe hizo za kufana.
Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni waiziri wa Elimu Julius Ogamba,waziri wa kawi Opiyo Wandayi,Gavana wa Kisumu Anyang Nyong’o, na Katibu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Stephen Isaboke, miogoni mwa viongozi wengine.