Kundi la kwanza laekea Ghana kwa mashindano ya Riadha Afrika

Dismas Otuke
1 Min Read

Kundi la kwanza la wanariadha 36 na maafisa watano wa timu ya Kenya, limeondoka nchini mapema Jumamosi kuelekea Acrra,Ghana, kwa makala ya 24, ya mashindano ya riadha ya Afrika, yatakayoandaliwa kati ya Mei 12na 17.

Timu hiyo imekuwa ikifanya mazoezi katika uwanja wa Nyayo,kujiandaa kwa mashindano hayo .

Kikosi cha Kenya kitakachoshiriki kwa mbio na mashindano ya uwanjani kinawajumuisha wanariadha 74.

Kenya italenga kuboresha matokeo ya mwaka 2024 mjini Doaula,Cameroon, ilikomaliza ya pili kwa medali 19,dhahabu 5,fedha 7 na shaba 7, nyuma ya Afrika Kusini.

Share This Article