Rais wa Marekani Donald Trump, amesema mapigano kati ya Russia na Ukraine yatakamilika katika muda wa siku tatu.
Muda mfupi baada ya tangazo la Trump, Rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky alithibitisha kumalizika kwa vita hivyo licha ya pande zote kulaumiana kuhusu kukiuka mkataba wa kusitisha vita hivyo.
Katika ujumbe wake, Trump alisema aliomba binafsi usitishaji huo wa mapigano wa siku tatu na akitumai maombi yake yatakubaliwa na Rais Vladimir Putin na Rais Volodymyr Zelensky.
Putin alikuwa ametangaza usitishaji wa mapigano tarehe 8 hadi 9 Mei kabla ya maadhimisho ya Siku ya Ushindi yaliyopangwa kufanyika Jumamosi.
Hata hivyo Kyiv hapo awali ilikuwa imetoa wito wa usitishaji wa mapigano usio na kikomo kuanzia tarehe 6 Mei.