Chief Godlove amtambulisha Chocolate

Msanii huyo wa kike kwa jina Chocolate tayari ana albamu kwa jina Queen of Bongo Fleva.

Marion Bosire
2 Min Read

Mfanyabiashara bilionea wa Tanzania, mshawishi wa mitandao, mhisani na mganga wa kiroho Chief Godlove amemtambulisha msanii wake mpya aitwaye Chocolate.

Msanii huyo wa kike anakuja akiwa tayari na albamu nzima ya nyimbo saba.

“Nakukaribisha kwenye ulimwengu wa mziki @chocolategirltz Tanzania na Watanzania wamesubiri kuona uwezo wako nenda kawaonyeshe uwezo wako kwa huu mziki wako sioni Kama kuna haja ya mimi kupiga piga kelele,” aliandika Godlove.

Chief ambaye anamiliki kampuni ya muziki ya Chief Loot, alisema kwamba atakuwa tu anamsaidia Chocolate kuafikia upeo kama msanii akisisitiza kwamba yeye ni msanii wa Watanzania na wala sio msanii wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chocolate alijitambulisha akisema jina lake halisi ni Agness Silvester Samson akitangaza albamu yake iitwayo “Queen of bongo flavour” inayopatikana kwenye majukwaa yote ya mtandaoni.

Binti huyo alitaja wasanii wa muda mrefu wa Bongo Fleva kama Dully Sykes na Barnaba Classic ambao alishukuru kwa kukubali kumsaidia kikazi.

“Shukrani zangu za mwisho ziende kwa Chief Godlove pamoja na team nzima ya Chief loot Music vipaji vilikua vingi Lakini wakaniona mimi” aliandika chocolate kwenye Instagram.

Huyu sio msanii wa kwanza ambaye Chief Godlove anamtambulisha, aliwahi kumtambulisha msanii kwa jina, Pipijojo ambaye kwa sasa ni msanii wa kampuni ya Nandy iitwayo The African Princess.

Share This Article