Rais Ruto kuhutubia Bunge la Tanzania Jumanne

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Kenya William Ruto.

Rais wa Kenya William Ruto ambaye yuko kwenye ziara ya siku mbili ya kiserikali nchini Tanzania,  leo Jumanne anatarajiwa kulihutubia Bunge la Tanzania.

Hotuba ya Rais Ruto kwenye bunge hilo inatarajiwa kuangazia umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili za Afrika Mashariki.

Hayo yanajiri saa chache baada ya nchi hizo mbili kutia saini Mikataba Nane ya Maelewano, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta tofauti.

Akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba hiyo, Rais Ruto alisema mikataba hiyo inabuni mikakati mipya ya ushirikiano katika sekta za miundombinu, biashara, usafiri wa kikanda, utumishi wa umma, usalama na nishati.

Aidha, Rais Ruto na mwenyeji wake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, walikariri kujitolea kwao kuboresha ushirkiano wa kimkakati kwa manufaa ya nchi hizo mbili.

Share This Article