Mbio za Dunia za kupokezana kijiti zitaanza leo mjini Gaberone, Botswana, huku Kenya ikiwakilishwa na timu tano.
Kenya itashiriki katika fani za mita 100 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti wanaume , mita 100 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti jinsia mchanyato,mita 400 wanaume,mita 400 wanawake na mita 400 wanaume na wanawake kupokezana kijiti.
Kenya ilishinda medali ya shaba katika Makala ya mwaka jana mjini Guanzou,Uchina.
Mashindano hayo yataandaliwa Jumamosi na Jumapili na yanafanyika Afrika kwa mara ya kwanza.
Timu nane bora ziotafuzu kwa mashindano ya Riadha Ulimwenguni mwaka ujao huku timu mbili zikifuzu kwa mashindano ya dunia ya Ultimate yatakayofanyika baadaye mwaka huu.