Ahly na Zamalek, kumenyana leo katika derby ya Cairo

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa mara 45 wa Ligi Kuu nchini Misri, Al Ahly, watashuka dimbani Cairo, leo Ijumaa usiku katika derby  dhidi ya watani wa jadi Zamalek, itakayobaini hatima ya timu zote mbili.

Ahly, hawana budi kupata ushindi ili kuwa na matumaini ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao huku Zamalek, wakihitaji ushindi ili kukaribia kutawazwa mabingwa wa ligi kwa mara ya 15.

Zamalek wanaongoza jedwali kwa pointi 50, zikisalia mechi tatu, wakati Ahly, wakishikilia nafasi ya tatu kwa alama 44.

Ahly, ambao wamekuwa na msimu mbovu watahitaji kushinda mechi zote zilizosalia dhidi ya Enppi, nyumbani Cairo Mei 5, na hatimaye ugenini dhidi ya Al Masry, tarehe 15 mwezi huu, na kutarajia Pyramids ,watateleza ili wafuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Mwamuzi wa Cairo Derby Matthias Jollenbeck kutoka Ujerumani

Ahly, maarufu kama Red Devils, wameshinda derby hiyo katika ligi mara 51, wakati Zamalek, wakishinda mechi 29 , na nyingine 51, zikimalizikia sare.

Mechi hiyo itasimamiwa na mwamuzi wa kiutoka Ujerumani, Matthias Jollenbeck, aliyeteuliwa na chama cha soka nchini Misri- EFA.

Share This Article