Rais Ruto amtuza Sawe shilingi milioni 8 na gari

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amemtuza mshikilizi wa rekodi ya dunia ya marathon Sabastian Sawe, shilingi milioni 8 pamoja na gari .

Ruto amemtuza Sawe mapema Alhamisi alipompokea katika Ikulu ya Nairobi, akikariri kujitolea kwa serikali kuboresha sekta ya michezo nchini.

Upande wake Sawe amesema kuwa ushindi wake ni kwa ajili ya wakenya wote, huku akiipongeza serikali kwa kuunga mkono michezo nchini.

Pesa alituzwa Sawe zinajumuisha shilingi milioni 5, kwa kuvunja rekodi ya dunia na shilingi milioni 3, ambazo hutuzwa mshindi wa medali ya dhahabu.

Aidha, Ruto ameahidi kumnunulia Sawe gari chaguo lake mwenyewe lenye nambari za usajili 1:59:30, ambao ni muda wa rekodi mpya ya dunia aliyoiweka.

Hafla hiyo imehudhuriwa na familia ya Sawe wakiwemo wazazi wake,Waziri wa michezo Salim Mvurya, na pia kinara wa chama cha Riadha Kenya,Jackson Tuwei.

Share This Article