Mshikilizi wa rekodi mpya ya dunia katika mbio za marathon, Sebastian Sawe, anatarajiwa kuwasili jijini Nairobi leo Jumatano usiku, siku mbili tu baada ya kuvunja rekodi ya dunia.
Sawe, aliye na umri wa miaka 30, alivunja rekodi ya dunia ya saa 2 na sekunde 35, ya marehemu Kelvin Kiptum mwaka 2023.
Mwanariadha huyo wa Adidas aliweka rekodi mpya ya dunia ya saa 1 dakika 59 na sekunde 30, akiwa mwanaume wa kwanza kukamilisha marathon chini ya muda wa saa mbili.
Ndege ya Kenya Airways atakayosafiria Sawe, inatarajiwa kutua uwanja wa JKIA saa mbili na dakika 35 usiku.