Klabu ya AFC Leopards imetangaza kuwa iliuza tiketi 20,336, katika derby ya 99 ya Mashemeji iliyopigwa Jumapili uwanjani Nyayo.
Leopards ambao walikuwa wenyeji wa mechi hiyo ya Ligi walipoteza bao moja kwa bila dhidi ya Gor Mahia, na kufifisha matumaini yao ya kunyakua taji ya ligi kuu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998.
Kufuatia ushindi huo Gor wanaongoza jedwali kwa alama 61 ,pointi 5 zaidi ya watani wao Leopards wanaoshikilia nafasi ya pili.
Mashabiki walifurika uwanjani Nyayo kwa derby hiyo.