Jeshi la Mali- FAMa, ladhibiti hali baada ya kukabiliana na magaidi

Dismas Otuke
1 Min Read

Majeshi ya Mali  (FAMa) yametangaza kudhibiti hali nchini humo baada ya kukabiliana na magaidi  kutibua mipango yao kadhaa ya kutekeleza mashambulizi yaliyolenga miji mbalimbali.

Kulingana na taarifa rasmi  kutoka kwa mkuu wa jeshi ,jeshi hilo liliwaangamiza magaidi kadhaa kwenye makabiliano hayo ya Jumamosi.

Magaidi hao walitekeleza mashambulizi ya angani katika maeneo ya mijini  lakini majeshi ya Mali yaliwakabili kabla ya kusababisha uharibifu mkubwa.

Kufukia Jumamosi jioni majeshi hayo yaliendeleza msako ili kuwaondoa magaidi hao ambao wamekuwa tishio kwa raia.

Serikali ya Mali imewataka raia wake nchini humo na pia walio katika mataifa ya kigeni kutahadhari .

TAGGED:
Share This Article