Korir na Lokedi watetea ubingwa wa Boston Marathon

Korir alichomoka na kuchupa kileleni kutoka umbali wa kilomita 34, na kukakata utepe kwa saa 2 dakika 1 na sekunde 52,akivunja rekodi ya mwaka 2011 yake Mkenya mwenza Geofrey Mutiso.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wakenya John Korir na Sharon Lokedi wametetea mataji ya mbio za Boston Marathon wakati wa makala ya 130 ,yaliyoandaliwa Jumatatu jioni nchini Marekani.

Korir alichomoka na kuchupa kileleni kutoka umbali wa kilomita 34, na kukakata utepe kwa saa 2 dakika 1 na sekunde 52,akivunja rekodi ya mwaka 2011 yake Mkenya mwenza Geofrey Mutiso.

Bingwa wa dunia Felix Simbu wa Tanzania alimaliza wa pili kwa saa 2 dakika 2 na sekunde 47 ,huku Benson Kipruto pia wa Kenya akihitimisha nafasi tatu bora kwa saa 2 dakika 2 na sekunde 50.

Lokedi pia ametetea taji ya wanawake akiibuka mshindi kwa saa 2 dakika 18 na sekunde 51,huku Wakenya wakitwaa nafasi tatu bora.

Loice Chemnung amechukua nafasi ya pili huku Mary Ngugi akiridhia nafasi ya tatu.

Share This Article