Mwimbaji na mcheza densi wa Uganda Nakato Sandra maarufu kama Sandra Naxx amevunja ukimya wake kufuatia kuvuja kwa video zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii.
Mwimbaji huyo alionyesha utulivu katika chapisho fupi kwenye majukwaa yake ya mitandao ya kijamii, huku picha kutoka kwenye video hizo zikisambaa kwa kasi kwenye majukwaa mbalimbali.
Aliandika ujumbe mfupi wa uthabiti Jumamosi mchana akisema, “Wanaogopa uwezo wangu,” akirejelea moja kwa moja suala la video zilizovuja.
Video hizo zilisababisha aangaziwe kwa njia ambayo hakutarajia ikitizamiwa kwamba yeye ni msanii chipukizi ambaye alipata umaarufu kwanza kupitia ustadi wake wa kipekee wa kucheza densi kabla ya kuhamia kwenye muziki.
Katika moja ya video hizo, Sandra Naxx anaonekana nusu uchi, akiwa amevaa vazi jeupe la ndani, huku akicheza wimbo wa msanii wa dancehall kutoka Jamaica, Spice, unaoitwa “So Mi Like It.”
Video nyingine inaonyesha akijiweka kimakusudi kwa ajili ya hadhira aliyokusudia.
Kazi ya muziki ya mwimbaji huyo ilikuwa ikipata mafanikio, huku wimbo wake wa ushirikiano na Alien Skin “Kapati” ukifanya vizuri kwenye majukwaa ya muziki.
Hata hivyo, kuvuja kwa video hizo kumeathiri pakubwa taswira yake inayokuwa.
Huku anayehusika na uvujishaji wa video hizo akiwa bado hajajulikana, Sandra Naxx au timu yake ya usimamizi hawajatoa taarifa rasmi kuhusu suala hilo zaidi ya chapisho lake la mitandaoni.