Vipusa wa Uganda waingia raundi ya pili kufuzu Kombe la Dunia

Dismas Otuke
0 Min Read

Timu ya Uganda kwa wasichana wasiozidi umri wa miaka 17, imefuzu kwa raundi ya pili kuwania tiketi kushriki fainali za Kombe la Dunia licha kutoka sare tasa Jumamosi dhidi ya Zimbabwe jijini Kampala.

Uganda walifuzu kwa raundi ya pili ambapo watamenyana  na Kenya baada ya kushinda duru ya kwanza mabao 2-0 mjini Harare Zimbabwe.

Fainali za Kombe la Dunia zinatarajiwa kuandaliwa nchini Morocco mwishoni mwa mwaka huu.

Share This Article