Miamba wa soka nchini AFC Leopards wameambulia kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa mabingwa watetezi wa Ligi kuu Kenya,Police FC, katika mojawapo ya mechi zilizochezwa Jumamosi.
Police FC walidhihirisha ubora wao katika mechi hiyo uwanjani Nyayo,dhidi ya Ingwe wakiongoza 3-0 kufikia mapumziko kupitia kwa mabao ya Vyes Koutiama dakika ya 7,Eric Zakayo dakika ya 31 na Charles Ouma dakika ya 45.
Kipigo hicho kimetia dosari safari ya Ingwe kunyakua ubingwa wa Ligi ya Kenya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998,wakisalia katika nafasi ya pili alama 2 nyuma ya viongozi Gor Mahia ,walio na mechi moja mkobani.
Gor na Ingwe zitamenyana wikendi ijayo kwenye derby ya Mashemeji ambayo huenda ibaini mwelekeo wa ligi ifikiapo mwishoni mwa msimu.
Gor wangali wanashikilia kukutu msimamo kwa alama 57 zikisalia mechi 7.