Bunge la Tanzania laidhinisha bajeti ya Afisi ya Rais

KBC Digital News
1 Min Read
Kikao cha Bunge la Tanzania. Picha/Hisani.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepitisha bajeti ya Ofisi ya Rais, Ikulu na Usimamizi wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora, yenye jumla ya shilingi trilioni 1.5 kwa ajili ya ofisi hiyo katika mwaka wa fedha 2026/2027.

Bajeti hiyo imewasilishwa bungeni jijini Dodoma Aprili 17, 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Usimamizi wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete na kisha kujadiliwa na wabunge kabla ya kupitishwa rasmi.

Awali wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti hiyo, Ridhiwani amesema kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 1.4 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, huku shilingi bilioni 163 zikielekezwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Share This Article