Iran yafungua Mlango Bahari wa Hormuz

Mlango huo utakuwa wazi kwa muda wa siku 10 za kusitisha mapigano nchini Lebanon.

Tom Mathinji
1 Min Read
Iran yafungua mlango bahari wa Hormuz.

Serikali ya Iran imetangaza kufunguliwa kwa mlango bahari wa Hormuz, hatua inayotoa fursa kwa meli za kibiashara kupita.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema kuwa mlango huo utakuwa wazi kwa muda wa siku 10 za kusitisha mapigano nchini Lebanon.

Aidha, Araghchi amesema Tehran inapinga makubaliano  ya muda ya kusitisha mapigano, akisisitiza kuwa vita vinapaswa kukomeshwa kabisa katika eneo hilo.

Hayo yanajiri huku Rais wa Marekani  Donald Trump akidokeza kuwa Mlango-Bahari unasalia kuwa wazi, lakini kizuizi cha majini cha Marekani dhidi ya Iran kitabaki mahali pake hadi makubaliano ya mwisho ya amani yatakapoafikiwa.

Mapema wiki hii Marekani ilikuwa imetangaza kuwa imeanza kutekeleza kizuizi cha kijeshi katika bandari za Iran na mlango bahari wa Hormuz.

Trump alitangaza usitishwaji wa mapigano nchini Iran kwa muda wa wiki mbili ili kutoa nafasi kwa mazungumzo ya amani kufanyika. Muda wa usitishwaji huo unakamilika tarehe 22 mwezi Aprili.

Share This Article