Sekta ya Utalii humu nnchini imepigwa jeki pakubwa kufuatia kuzinduliwa kwa mfumo mpya wa kidijitali kupitia mtandao.
Akizungumza wakati wa kuzinduliwa kwa TouristTap,Waziri wa Utalii Rebecca Miano, alisema mfumo huo utarahisisha shughuli za kitalii humu nchini na kuongeza pato la kitaifa.
Sekta ya utalii ilichangia pakubwa pato la kitaifa ikukasanya takriban shilingiu bilioni 500 mwaka uliopita na pia hutoa nafasi za ajira zipatazo milioni 3.
Mfumo huo wa malipo utarahisisha shuhguli za Utalii kama vile ada za kuingia mbugani,kununjua bidhaa sokoni,kulipia gharama za usafiori,kulipia mikahawa,ada za uwanja wa ndege na hata wachuuzi.
App hiyo imetengenezwa na kampuni ya Craft Silicon.